Breaking News
recent

YALIOJIRI MKUTANO NA WANAHABARI YANGA

Taswira inaweza kujumuisha: Watu 2, watu wanakaa
Uongozi wa klabu ya Yanga umepeleka malalamiko kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ukipinga uamuzi wa Bodi ya Ligi kumfungia kocha Mwinyi Zahera mechi tatu kutokana na shutuma za upendeleo alizotoa kwa Bodi hiyo baada ya mchezo kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting
Katika mchezo huo wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu,kocha Zahera alilalamikia hatua ya Bodi ya Ligi kukataa kusogeza mbele kwa siku mbili mechi dhidi ya Ruvu Shooting hasa ikizingatiwa Yanga ilipaswa kusafiri kutoka Botswana
Yanga tulicheza Botswana August 24 na tukasafiri kurejea nchini usiku wa kuamkia August 26, wachezaji walipumzika siku moja tu kabla ya kushuka tena dimbani
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema adhabu ya kumfungia kocha mechi tatu ni kubwa pengine faini ingetosha
Pamoja na adhabu hiyo, Kocha wetu alipigwa faini ya kulipa laki tano kutokana na mavazi aliyovaa kwenye mchezo huo
Hata hivyo wengi tumeshangazwa na uamuzi huo kwani pamoja na adhabu kumkumba yeye, kocha msaidizi wa Ruvu Shooting nae hakuwa na mavazi rasmi lakini hakuadhibiwa
Mwakalebela amesema hawaoni kama Bodi ya ligi imemtendea haki Zahera
"Unapomfungia kocha mechi tatu kwa nini usimpe faini tu aendelee kufundisha timu?," amehoji Mwakalebela
"Tumeshaiandika barua Wizara kulalamikia haya madhaifu na tunasubiri majibu"
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.