Breaking News
recent

Samuel Eto’o ameamua kustaafu soka

Taswira inaweza kujumuisha: Mtu 1, ndevu


Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Samuel Eto’o ameamua kutundika njumu zake baada ya kusakata kabumbu kwa miaka 22.
Eto’o, 38, alianzia Real Madrid ambapo alicheza mechi tatu tu. Alipoondoka hapo alichezea timu 13, ikiwemo Barcelona, Inter Milan, Chelsea, Everton na Sampdoria.
Eto’o anahusishwa zaidi na Barcelona kwa sababu aliwasaidia vigogo hao wa Spain kushinda makombe matatu ya La Liga na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Baada ya miaka mitano ya kuwa na Barcelona, alijiunga na Inter Milan, mwaka 2009, ambapo alishinda tena Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya tatu, safari hii akiwa chini ya kocha Jose Mourinho.
Eto’o pia alicheza kwa muda mfupi katika Ligi Kuu ya England, akiwa na Chelsea na Everton.
Alitangaza siku ya Ijumaa kupitia Instagram kuwa ameamua kustaafu kucheza soka baada ya kuondoka Qatar SC mapema mwaka huu.
Aliandika: “Mwisho. Naelekea kwenye changamoto nyingine. Asanteni nyote, nawapenda sana.”
Baada ya kuitwa katika timu ya taifa ya Camerron siku moja tu kabla ya kutimiza umri wa miaka 16, Eto’o aliichezea Cameroon mara 118 akipachika mabao 56.
Aliisaidia Cameroon kushinda medali ya Dhahabu mwaka 2000 kwenye michuano ya Olimpiki nchini Australia, na pia kushinda Afcon mwaka 2000 na 2002.
Eto’o ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara nne.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.