Breaking News
recent

C.E.O MPYA WA SIMBA ATANGAZWA. Ni kutoka Africa Kusini

Taswira inaweza kujumuisha: Watu 2

Klabu ya Simba SC imemtambulisha rasmi Senzo Mazingiza kutoka Nchini Afrika Kusini kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa klabu hiyo, akichukua nafasi ya Crescentius Magori anayemaliza muda wake.
_
"Simba ni timu kubwa sana, nimekuwa naifuatilia kwa muda sasa, nimejifunza kuwa ni timu kubwa na tunaweza kuifanya kuwa kubwa zaidi, sio tu ukanda wa Afrika Mashariki bali kuwa klabu kubwa zaidi Afrika"-CEO mpya Senzo Mazingiza
_
"Kuanzia wiki ijayo nitakuwa CEO mstaafu, nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipa, nawashukuru sana Wanasimba Kwa tuliokwazana niwaombe radhi ilikuwa sababu ya kazi yangu"-CEO anayemaliza muda wake, Crescentius Magori.

Taswira inaweza kujumuisha: Mtu 1
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.