Breaking News
recent

Uhamisho wa wachezaji England wazifanya vilabu vya EPL kutumia £1.41bn

Kieran Tierney, Alex Iwobi, Ryan Sessegnon na Ismaila SarrHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKieran Tierney, Alex Iwobi, Ryan Sessegnon na Ismaila Sarr
Usajili wa wachezaji dakika za mwisho ulivifanya vilabu vya Ligi ya Premia kutumia hadi £1.41bn, karibu kufikia rekodi ya £1.43bn iliyowekwa 2017, kwamujibu wa kampuni ya uhasibu ya Deloitte.
Fedha zilizotumiwa na vilabu vikubwa siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji ilikua £170m -kukamilisha mikataba 17 pekee, ikilinganishwa na idadi ya uhamisho wa siku ya mwisho kutoka tangu 2009.
Hatua ya Everton ya kumsajili kwa £34m mshambuliaji Alex Iwobi kutoka Arsenal imetajwa kuwa mkubwa, huku uhamisho huo pia ukimsaidia Romelu Lukaku kuondoka kwenda kwa kima cha £74m - hasara ya £1m ya ada waliolipa Everton.
Arsenal walitumia jumla ya £155m kuwanunua wachezaji kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Siku ya mwisho ya ya shughuli hiyo ilitumia £25m kumnunua beki wa kushoto wa Celtic Kieran Tierney na £8m kumnyakua beki wa ka Chelsea David Luiz.
Tottenham ilimsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa Real Betis Giovani lo Celso pamoja na winga Fulham Ryan Sessegnon kwa £25m.
Watford ilivunja rekodi ya matumizi yake inayoripotiwa kuwa £25m, kumnunua winga Ismaila Sarr nayo Leicester ikajipatia mshambuliaji wa kati wa Sampdoria Dennis Praet kwa £18m.
Alex IwobiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wachezaji watatu wa zamani wa kimataifa walihama - Burnley ilimsajili kingo wa kati wa Chelsea Danny Drinkwater na Manchester City wakamchukua kipa wa Derby Scott Carson, wote kwa mkopo, huku Newcastle wakimsajili tena mshambuliaji Andy Carroll bila malipo.
Huu ulikua mwaka wa pili mtawalio kwa vilabu vya Ligi Kuu ya Premia kuwasajili wachezaji siku ya mwisho ya kba ya msimu kuanza, badala ya mwisho wa mwezi Augosti.
Vilabu vikubwa vilishindwa kufikia muda wa mwisho wa kufungwa kwa dirisha la usajili, lakini timu kutoka Scotland, Ligi ya kwanza na ya pili zote kutoka ligi kuu ya mataifa ya Ulaya zina hadi tarehe 2 Septemba kuwanunua wachezaji .
Idadi jumla ya wachezaji waliosajiliwa katika ligi kuu ya England msimu huu ilishuka kwa mwaka wa sita mtawalio.
Mikataba ipi ilifikiwa msimu wa joto?
Vilabu 20 vya ligi ya England vilivunja rekodi zao za uhamisho msimu huu, huku with Sheffield United wakivunja rekodi yao mara nne.
Arsenal, Aston Villa, Leicester (mara mbili), Manchester City, Newcastle, Southampton, Tottenham, Watford - siku ya mwisho ya uhamisho - West Ham na Wolves ni wengine 10.
Uhamisho wa Harry Maguire wa £80m kutoka Leicester kwenda Manchester United ndio ulikua usajili wa bei ghali zaidi msimu huu, ukifuatiwa na ule wa Arsenal wa £72m kumnunua winga wa Lille Nicolas Pepe.
Mabingwa Manchester City walimnunua kiungo wa kati wa Atletico Madrid Rodri kwa kima cha £62.8m nao Juventus wakamnunua beki wakulia -nyuma Joao Cancelo kwa £60m.
Spurs walitumia £53.8m kumsajili kungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele - usajili wa kwanza wa kikosi chao cha kwanza tangu January mwaka 2018.
Wachezaji 10 walionunuliwa kwa kitita kikubwa na vilabu vyakwa Premier League msimu huu
Most expensive Premier League signings this summer
Villa walitumia £125m, klabu ya pili kubwa kugongakufika kiwango hicho baada ya Fulham,amabo msimu uliopita na baadae wakashushwa daraja mwezi April.
Uhamisho mwingine mkubwa ulikuwa wa beki wa kulia nyuma wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka (£50m kutoka Crystal Palace), Mshambuliaji wa West Ham Sebastien Haller (£45m kutoka Eintracht Frankfurt), Mshambuliaji wa Newcastle Joelinton (£40m kutoka Hoffenheim) na wa kiungo wa kati wa Leicester Youri Tielemans (unaoripotiwa kuwa £40m kutoka Monaco).
Chelsea pia walitumia £40m kumnunua Mateo Kovacic kutoka Real Madrid licha ya kuwa na marufuku ya uhamisho wa wachezaji.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Croatiatayari alikuwa anacheza kwa mkopo, kwa hivyo Chelsea chini ya ukufunzi wa kocha Frank Lampard waliruhusiwa kumnunua kwa sababu alikuwa amesajiliwa.
Hatua yao ya kumuuza Eden Hazard, Real kwa kima cha £89m, iliyohusisha pia kuongezeka kwa kima hicho hadi £150m, ilikuwa moja ya mikataba mikubwa kufikiwa duniani
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.