Breaking News
recent

Tanzanite yatinga fainali Cosafa

WINFRIDA MTOI
TIMU ya Taifa ya Wanawake chini ya umri wa  miaka 20, Tanzanite, imetinga fainali katika michuano ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa), baada ya kuwachapa mabao 2-0  wenyeji Afrika Kusini.
Mchezo huo wa nusu fainali ulipigwa jana kwenye  Uwanja wa Gelvandale, Port Elizabeth, Afrika Kusini. Mabao ya Tanzanite yalifungwa na  Enekia Kasonga dakika ya 18 na Opa Clement dakika ya 30.
Kwa matokeo hayo,  Tanzanite itakutana na Zambia, katika mchezo wa fainali utakaopigwa keshokutwa kwenye uwanja huo, timu zote zikitokea kundi A.
Tanzanite ambayo imealikwa katika michuano hiyo, walifanikiwa kutinga nusu fainali, baada  ya kuichapa mabao 2-1  Botswana  kabla ya kupata ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Eswatini, kisha kufungwa na Zambia mabao 2-1.
Akizungumza  kutoka Afrika Kusini baada ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Tanzanite, Bakari Shime, aliwapongeza wachezaji wake kwa kufuata maelekezo aliyowapa na kufanikiwa kufikia malengo waliyojiwekea.
Shime alisema katika mchezo huo walijua wanakutana na wenyeji, pamoja na kucheza mechi mfululizo, lakini walitumia nguvu kubwa hadi kufanikiwa  kufikia hapo.
Alisema kuelekea mchezo wa fainali, wanakwenda kufanyika kazi kasoro zilizojitokeza ili wapinzani wao wasiwafunge tena mara ya pili kama walivyokutana kwenye makundi.
“Nashukuru tumefika fainali na ndiyo ilikuwa malengo yetu, nawapongeza wachezaji wangu kwa kujituma, tunafurahia kufiki yale tuliyokuwa tumejiwekea,” alisema Shime.
Alieleza kuwa itakuwa ngumu kwa Zambia kuwafunga tena kwa mara ya pili kwa sababu baada ya kuingia fainali, wachezaji wamekuwa na  morali kubwa,atakaa nao  kuwaeleza kitu cha kufanya katika mchezo huo.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.