Breaking News
recent

Rajab Abdul Kahali jina maarufu Harmonize awasilisha ombi la kujiondoa Wasafi

Harmonise
Msanii Rajab Abdul Kahali kwa jina maarufu Harmonize hatimaye ameandika rasmi kwa kundi la Wasafi Classic Baby WCB akitaka kandarasi yake kuvunjwa.
Akizungumza na runinga ya Wasafi, afisa mkuu mtendaji wa WCB Sallam SK alias Mendez alifichua kwamba msanii huyo ameandika rasmi kwa kundi hilo akisema anataka kujiondoa.
Sallam amesema kwamba kwa sasa moyo wa msanii huyo haupo tena na WCB na ameitisha mkutano na usimamizi wa WCB katika harakati yake ya kukubaliana na hatua hiyo.
"Harmonize kwa sasa moyo wake haupo WCB, kimkataba bado yupo. Kwa nini nasema hivo? Harmonize ameshatuma barua ya maombi ya kuvunja mkataba na yuko tayari kupitia vipengele vyote vya sheria kusitisha mkataba wake na ni kitu ambacho tumependezewa nacho. Yeye mwenyewe ameridhia na ameomba kikao na uongozi," alisema Sallam.
Harmonize na aliyekuwa meneja wake Mr. PuazHaki miliki ya pichaPUAZ
Hatahivyo amesema kwamba muimbaji huyo wa wimbo 'My Boo' bado yupo katika mkataba wa WCB na kusisitiza kwamba ingekuwa heri iwapo Harmonise angetoka bila kuzua zahama.
"Sisi kama taasisi ya WCB tuko radhi kwa kile ambacho ataamua, hatuwezi kupinga chochote. Akiamua kufuata maelezo hayo ana baraka asilimia 100 za Wasafi na akitaka kushirikiana na Wasafi wakati wowote tuko wazi. Wajua unapoondoka kwa mazingira mazuri inasaidia uhusiano usalie pale pale," alizungumza katika .
Kulingana na Sallam, tangazo hilo kwamba Harmonize amejiondoa rasmi WCB litatangzwa rasmi baada ya mchakato wote huo kufuatwa na kukamilishwa
"Siku ambayo atatoka kimkataba tutaangazia umma. Kwa sasa hivi ameandika barua. Nafasi yake imetoka WCB. Kufanya kazi ndani ya WCB, ndani ya moyo wake, haiko radhi tena," aliongezea Sallam.
Msanii wa bongo Fleva HarmonizeHaki miliki ya pichaHARMONIZE/ FACABOOK
Sallam amesema katika tamasha la wasafi lililofanyika mjini Mwanza, kwamba Harmonise alitumia usafiri wa kibinafsi kufanya baadhi ya mambo yaliotoa tafsiri kwamba amejitenga.
''Alitufanyia mambo mengi ambayo hatukutarajia ikiwemo kumsimamisha msanii ambaye hana kibali chetu. Sisi hatupendi kuleta matabaka katika kundi letu lakini kama ilivyokuwa Harmonise aliingia kivyake, sio kwamba Diamond hawezi kufanya hivyo au Rayvany ni ile heshima kwamba WCB ina umoja na kwamba tunafuata sheria zilizopo''.
''Hatahivyo tumependezwa na hatua yake kwa sababu labda kuna vitu ameona akivifanya atafika mbali'', amesema Sallam akinukuliwa na gazeti la Mwananchi Tanzania.
Kuhusu kujitenga na wenzake Sallam amesema kwamba: Hili jambo sio sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo.
Maudhui ya Wasafi festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuandamana na wasanii wenzake ambao wapo katika tamasha ni kwenda kinyume.
Meneja huyo amewaomba radhi wasanii wote walioshiriki tamasha la Mwanza kutokana na Harmonise kufanya jambo hilo na kwamba uongozi wa Wasafi haukuwa na taarifa.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

1 comment:

  1. Borgata Hotel Casino & Spa (AtlanticCity) - JT Marriott
    Find 광명 출장마사지 rooms from $149+ at Borgata Hotel 군포 출장샵 Casino & Spa in Atlantic 부천 출장마사지 City, NJ. Compare room types 전라남도 출장샵 and prices from 영주 출장마사지 JT Marriott.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.