Breaking News
recent

Pepe kusugua benchi Arsenal

LONDON, England
HUENDA mashabiki wa Arsenal wakachelewa kumuona winga wao mpya, Nicolas Pepe, akianza kuitumikia timu yao msimu huu, kwa kile kinachoonekana kuwa bado hayupo fiti.
Kutokana na hilo, mchezaji huyo aliyeweka rekodi ya kusajiliwa kwa bei kubwa Arsenal, ataukosa mchezo dhidi ya Newcastle keshokutwa, Jumapili.
Imeelezwa kuwa staa huyo wa Ivory Coast hayupo fiti kikamilifu, huku Arsenal ikianza kumtengeneza vizuri kwa ajili ya kumwongezea nguvu zaidi ili aendane na soka la England.
Pepe anaonekana kuwa na mwili usiojitosheleza kwa soka la nguvu hasa atakapokutana na mabeki wagumu wa Ligi Kuu England, na tayari ameshaambiwa na kocha wake kuwa atahitaji muda hadi atakapokuwa tayari.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.