Breaking News
recent

Mpango wa chakula cha Beyoncé wakosolewa

BeyonceHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Utaratibu wa mlo anaoufuata muimbaji nyota wa Marekani Beyoncé "huenda ni wa hatari," muungano wa lishe bora na hali ya maisha nchini Uingereza umeiambia BBC.
Watu waliojisajili kupata utaratibu huo wa siku 22 hulipa $14 kupata maelezo kuhusu mlo unatokana na mapishi ya mboga tupu.
Lakini mtaalamu wa lishe bora Daniel O'Shaughnessy anasema utaratibu huo unaweza ukasababisha "mapungufu ya lishe bora mwilini".
Mratibu wa mazoezi na lishe ya Beyoncé, Marco Borges amesema muimbaji huyo "anatambua umuhimu wa lishe bora na mazoezi".

Ninahisi njaa

Utaratibu wa awali uliundwa mnamo 2013 lakini muimbaji huyo sasa anapigia upatu chakula anachokipika jikoni mwake maarufu Beyoncé's Kitchen, utaratibu alioutumia katika kujitayarisha kurudi jukwaani katika tamasha la Coachella mnamo 2018 baada ya kujifungua watoto pacha.
Video ya matangazo iliopakiwa katika ukurasa wake katika mtandao wa YouTube mwezi uliopita inaanza kwa kumuonyesha akikwea katika ratili ya kupima uzito huku akisema uzito wake "ni kama jinamizi la wanawake wote".
Video hiyo imetazamwa mara milioni 1.7.
Beyoncé anasema pia ili kufikia malengo yake ni lazima ajinyime "mkate, vyakula yva wanga, sukari, maziwa, nyama samaki na pombe... na nahisi njaa". Aliufuata utaratibu huo kwa siku 44.
'Mkate wa mboga'
Utaratibu wake uliundwa na muasisi wa '22 Days Nutrition', Borges, ambaye Beyonce anamtambua kama "rafiki, mratibu mazoezi, na mtaalamu wa mazoezi na mhariri bora wa New York Times".
O'Shaughnessy amehoji faida zinazotajwa za kutokana na utaratibu huo katika lishe bora.
Mfano, mojawapo ya mapishi "mkate wa mboga" ulio na gramu 36 za protini, ulionekana kuwa na gramu 24 pekee, alisema.
Huku kinywaji cha mboga tupu, kikiwa na vijiko vinane vya sukari.

Bidhaa za wanyama

Idaraya huduma za afya Uingereza inapendekeza wanaume wale vyakula vyenye kalori 2,500 kwa siku na wanawake 2,000 - lakini utaratibu huo una kalori 1,400.
"Hiki ni kiwango kidogo kwa mtu yoyote, watumiaji watachoka hususan wanapoongeza na kufanya mazoezi," bwana O'Shaughnessy ameongeza.
"Huenda ikawa hatari kwa mtu wa kawaida kuufuatilia utaratibu huo pasi kuwepo na kikosi cha wataalamu wa lishe bora na pia wataalmu wa kufanyisha mazoezi kama alivyo nao Beyoncé."
Ukiondoa bidhaa zote za wanyama bila ya taarifa yoyote kuhusu masuala gani ya lishe bora mtumiaji anastahili kuzingatia, kama vile kupata mbadala wa vitamini B12, madini ya iron au protini, pia ni tatizo amesema O'Shaughnessy.
'Ni rahisi kuwa katika hatari ya kushawishika'
Na nyota kama Beyonce wanastahili kuwahimiza wanawake wajivunie miili yao.
"Beyoncé anauza ndoto," O'Shaughnessy anasema.
"hili linatia wasiwasi kwasababu ana vijana wengi wanaomfuata ambao wamo katika hatari ya kushawishika.
"Anaweza kuwafikia mamilioni ya watu."
Beyoncé hakujibu wito wa kutoa kauli kuhusu haya.
Katika taarifa yake, Borges, amesema: "Beyoncé alitumia mchanganyiko wa utaratibu wa chakula cha mboga tupu na mazoezi ya kila siku kwa nidhamu na bidii kubwa ili kufikia malengo yake binafsi katika kujitayarisha kwa tamasha hilo la Coachella...
"Aliyafikia malengo yake kwa ufanisi na alifanikiwa kujitokeza na kutumbuiza 100% katika tamasha lililolihitaji hilo.
"Anaendelea kutambua umuhimu wa lishe bora na mazoezi kama sehemu ya kuishi maisha yenye afya na furaha.
"Tunampongeza na ni hatua ya unyenyekevu yeye kuweza kueleza wengine kuhusu safari yake."
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.