Breaking News
recent

Harmonize awavuruga mashabiki

BAADA ya kutoa utambulisho kama msanii aliyesainiwa chini ya WCB katika ukurasa wake wa Instagram, staa wa Bongo Fleva, Rajab Kahali ‘Harmonize’, ameendelea kuwavuruga mashabiki zake wanaotaka kujua kama kweli ameondoka kwenye lebo hiyo.
Mara kadhaa, Harmonize amekuwa akikwepa kujibu kama bado yupo WCB au ametoka ingawa matendo yake yanaonyesha kama amejiweka mbali wasanii wa lebo hiyo kama vile kutoshiriki katika maonyesho ya Wasafi Festival na kujitengenezea utawala wake wa Konde Gang.
Akizungumzia hatua hiyo mmoja ya mameneja wa WCB, Mkubwa Fella alisema: “Kumzungumzia Harmonize sasa hivi nitasema uongo, mimi najua bado yupo Wasafi kwasababu ya mikataba ila yeye anaweza kusema anatakata kujitoa Wasafi.”
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.