Breaking News
recent

Ambokile afurahia maisha TP Mazembe


BAADA ya kutua katika Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, mshambuliaji wa zamani wa Mbeya City, Eliud Ambokile, amesema anafuarahia maisha ya ndani ya kikosi chake hicho.
Ambokile alisajiliwa na TP Mazembe Juni, mwaka huu, kwa mkataba wa miaka mitatu, baada ya dili lake na Black Leopads ya Afrika Kusini kushindwa kukamilika.
Akizungumza na BINGWA kutoka DR Congo, Ambokile alisema tayari ameshazoea mazingira ya klabu hiyo na hajiweki kama ni mgeni tena.
Ambokile alisema kazi iliyokuwapo mbele yake ni kupambana kuhakikisha anafanya vile vinavyomvutia kocha wake.
Alisema Ligi Kuu nchini humo inatarajia kuanza Ijumaa hii,  anajua ushindani uliopo na yuko tayari kupigania namba kikosini hapo.
“Si mgeni tena katika timu, hata chakula cha huku nimeshakizoea, najiandaa na Ligi Kuu natakiwa kupambana kwa sababu kila mchezaji ni mzuri, ila na mimi nimekuja kutafuta,” alisema Ambokile.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.