Wakati wamisri, waafrika na wapenda michezo duniani wakisubiri kuona nini atakachofanya Mohamed Salah katika Kombe la dunia 2018, miaka 84 iliyopita kulikuwa na shujaa wa kwanza wa mafarao na waafrika.
Abdelrehman Fawzi – alikuwa ndio mchezaji wa kwanza wa kiafrika kufunga goli katika mashindano ya kombe la dunia – alifunga magoli mawili katika mashindano ya 1934 kwenye mchezo ambao Misri walifungwa 2-4 na Hungary , Fawzi angeweza pia kuweka rekodi ya kuwa muafrika pekee kuwahi kufunga hat trick kama goli lake la 3 lisingekataliwa kimakosa na refa. Golikipa wa Egypt katika mchezo huo Mustafa Mansour anasema – wakati ubao ukisoma 2-2, Fawzi alichukua mpira kutoka katikati ya uwanja na kuwapiga chenga wachezaji wa Hungary na kwenda kufunga goli – refa akalikataa akisema ni offside.
Fawzi alizaliwa mnamo August 11, 1909 katika mji wa Port Said – Misri. Alivitumikia vilabu vya Zamalek na baadae akaenda kuitumikia Al Masry ambao wameitoa Simba katika CAF Confederation Cup hivi karibuni.
Fawzi alibaki kuwa mfungaji pekee wa goli/magoli wa kiafrika katika michuano ya kombe la dunia kutokea mwaka 1934 mpaka 1970.
Katika kipindi cha kutokea 1934-1970…. ilipita miaka 36 bila ushiriki wa timu za kiafrika katika kombe la dunia – Morrocco ikawa taifa la pili kushiriki katika michuano hiyo ndipo Houmane Jarir alipomrithi Fawzi kwa kuwa mfungaji mwingine wa kiafrika kwenye mashindano ya dunia.
Mfungaji bora wa wakati wa michuano ya dunia mpaka kufikia sasa ni Mghana Asamoah Gyan ambaye ana magoli 6, mawili kati ya hayo aliyafunga katika mashindano ya mwaka 2014.
Mchezaji wa mwisho wa kiafrika kufunga goli katika mashindano ya dunia ni mchezaji wa Algeria Abdelmoumene Djabou aliyefunga goli katika mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Ujerumani katika kombe la dunia 2014.
No comments:
Post a Comment