Breaking News
recent

ZAHERA AMVUA UNAHODHA YONDANI,AMPA AJIBU

ZAHERA
KOCHA wa Yanga, Raia wa Congo DR, Mwinyi Zahera amefanya maamuzi magumu baada ya kumvua unahodha beki kisiki wa timu hiyo, Kelvin Patrick Yondani na kumpa Ibrahim Ajibu leo Ijumaa, Januari 4, 2019.
Zahera amefanya maamuzi hayo baada ya Yondani kuingia mitini kwenye mazoezi ya leo bila kutoa taarifa yoyote kitendo ambacho Kocha huyo amesema kuwa hakifai kufanywa na mchezaji kiongozi kama Yondani.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari iliyoandikwa kwa kiswahili cha Congo ilisema; “Nimeamua kama tokea leo Kelvin Yondani…. namutoka Capitaine aiko tena Capitaine wa timu ya Yanga amebakiya muchezaji kama wengine wote.
“Sababu wakati unawapa wachezaji siku tano wapumuzike na siku ya sita umekosa mazoezi bila ata kupiga simu kwa mutu wowote umegoma mazoezi. Siwezi acha mutu kama ule mwenye aoneshe mfano kuwa Kapitaine. Naamua leo Kelvin aiko tena Capitaine na nimetiya Ibrahimu Ajibu kuwa Capitaine mupia wa Yanga.” amesema Zahera.

Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.