Breaking News
recent

Yeo Moriba: Mamake Paul Pogba kuwa balozi wa soka ya wanawake Guinea

Moriba Yeo ni mamake nyota wa klabu ya manchester United Paul Pogba

Shirikisho la soka nchini Guinea (Feguifoot) limemchangua mamake kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba kuwa balozi wa soka ya wanawake .
Uteuzi wa Yeo Moriba unajiri baada ya mkutano na rais wa shirikisho hilo Mamadou Antonio Souare.
Souare anatumai kwamba mchezaji huyo wa Ufaransa Paul na nduguze pacha , Florentin na Mathias, watamsaidia mama yao katika jukumu hilo jipya.
Moriba amewahi kuichezea timu ya soka ya wanawake nchini Guinea.
''Najivunia kile ambacho shirikisho la soka la Guinea na rais wake limefanya'', aliambia tovuti ya Feguifoot.
Yeo Moriba: Mamake nyota wa Man United Paul Pogba Haki miliki ya picha Getty Images
Florentin na Mathias ambao wote walizaliwa nchini Guinea wameichezea timu ya taifa ya Guinea Syli Nationale, kabla ya Moriba kuhamia Ufaransa ambako Pogba alizaliwa.
Beki Florentin mara ya mwisho alichezea klabu ya Genclerbirligi. Huku Naye mshambuliaji Mathias akiendelea kuichezea klabu ya Ufaransa Tours.
Matumaini ni kwamba familia hiyo itafanikiwa kuimarisha hadhi ya soka ya wanawake nchini Guinea.
Ikilinganishwa na wenzao wanaume , timu hiyo ya wanawake haijawahi kufuzu katika kombe la Afrika, kombe la dunia ama hata michezo ya Olimpiki.

Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.