Breaking News
recent

Brahim Diaz: Mfaham Kinda wa Man City aliyejiunga na Real Madrid kwa dau la £22m

Brahim Diaz sherehekea bao lake na Kevin de BruyneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDiaz alifunga magoli mawili dhidi ya Fulham katika kombe la Carabao mwezi Novemba
Manchester City inaendeleza sera yake ya kuwaruhusu vijana kujiendeleza kulingana na chanzo cha klabu hiyo.
Tayari klabu hiyo imeruhusu mchezaji wake kinda Brahim Diaz kujiunga na mabingwa wa ligi ya La Liga nchini Uhispania Real Madrid katika makubaliano yatakayogharimu £22m.
Ndio kinda wa hivi karibuni kuondoka katika klabu hiyo msimu huu, huku wachezaji wengi walioondoka wakishirikisha Jodon Sancho aliyehamia katika klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund kwa dau la £8m mwaka 2017.

Je Diaz ni nani na anacheza kiungo gani?

Umaarufu wa Diaz ulipanda wakati wa kombe la Uefa la vijana wasiozidi umri wa miaka 17 kule Azerbaijan wakati alipoifungia Uhispania magoli matatu na kuisadia kumaliza wa pili nyuma ya mabingwa Ureno baada ya kuishinda Uingereza katika robo fainali.
Wakati huo tayari alikuwa amejumuishwa katika kikosi cha City kilichopteza kombe la FA la vijana katika msimu wa 2016-2017 dhidi ya Chelsea.
Alianza kuichezea timu kubwa ya City mnamo mwezi Septemba 2016 na kutia saini kandarasi ya miaka mitatu siku chache baadaye.
Diaz mwenye urefu wa futi 5 na nchi 7, ana kasi ambayo ilitumika sana katika kiungo cha kati.
Tatizo la Diaz ni kwamba City tayari ina Raheem Sterling , Leroy Sane na Riyad Mahrez ambao wana uwezo wa kufanya kazi kama yake.

Je Diaz ataigharimu Real Madrid kitita cha pesa ngapi?

Real imekubali kulipa £5.5m kumnunua mchezaji huyo wa Uhispania pamoja na nyongeza ya £6.5m.
Kwa kuongezea, City ina kifungu cha kumnunua cha asilimia 15 ambayo itapanda hadi asilimia 40 iwapo Diaz ataondoka Real na kuelekewa Man United.
Diaz alijiunga na City kutoka klabu ya La Liga Malaga akiwa na umri wa miaka 14 mwaka 2013 na ameichezea klabu hiyo mara 15,mbali na mara nne msimu huu.
Brahim Diaz na Jadon SanchoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDiaz na Jadon Sancho, katika picha wakiichezea City 2017

Je City ina tatizo kuwahifadhi kinda wake wazuri?

Watasema hapana ushahidi kwamba mchezaji waliyetaka kumuhifadhi ni Phil Foden aliyetia kandarasi ndefu ya hadi 2024 Disemba.
City iliwauza baadhi ya wachezaji msimu uliopita akiwemo kipa Angus Gunn kwa klabu ya Southampton kwa dau la £13.5m, beki wa kulia Pablo Maffeo kwa klabu ya Stuttgart kwa dau la £9m na beki wa kushoto Angelino hadi PSV Eindhoven kwa dau la 15m.
Mwaka 2017, City ilimuuza mshambuliaji Kelechi Iheanacho kwa klabu ya Leicester kwa dau la £25m.
Duru zinaarufu kwamba hakuna uuzaji wa mchezaji uliofanywa kimakosa.

Je kitita kilichotolewa na Real Madrid ni kikubwa vipi?

City ilitaka kumzuia Diaz na kulikuwa na idadi kubwa ya maombi yaliowasilishwa katika juhudi za kumshawishi kusalia katika City.
Mwaka wa 2016 Diaz alisema kuwa atasalia Man City maisha yake yote.
Hatahivyo, wafanyikazi wa City pia wanakubali kwamba Real waliwasilisha ombi ambalo lilikuwa haliepukiki.
Je Diaz anaingiliana vipi katika mipango ya Real Madrid?
Pendekezo ni kwamba Diaz atakuwa katika kikosi cha kwanza cha msimu wote kabla ya uamuzi kuafikiwa kuhusu iwapo kuna mpango wa kumtoa kwa mkopo.
Hawahitaji wachezaji zaidi wa Uhispania katika mashindano ya klabu bingwa , kwa hivyo itasalia kuonekana iwapo atachezeshwa, Real ilikuwa imemsajili kinda mwengine wa Brazil Vinicius Junior kwa dau la£38.7m.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.