Breaking News
recent

Rais wa Ghana aamuru kukamatwa Rais wa chama cha soka

Rais wa Ghana Akufo Addoa metoa amri ya kukamatwa kwa Rais wa Ghana Football Association (GFA),  Kwasi Nyantekyi ambaye ni makamu wa kwanza wa Rais wa shirikisho la soka Afrika Caf.
Nyantekyi anatuhumiwa kufanya udanganyifu na ufisadi kwa kutumia jina la Rais la Rai wa Ghana Akufo Addoa.
Amri ya Rais Addo imekuja baada ya mwandishi wa habari Anas Aremeyaw kuibua udanganyifu na ufisadi wa Nyantekyi kupitia makala yake ya uchunguzi.
Uchunguzi huo pia unadaiwa kufichua vitendo vya ufisadi miongoni mwa maafisa wengine wa shirikisho la soka nchini Ghana.
Video hiyo inapangiwa kuoneshwa kwa wananchi Juni 6, 2018 lakini inadhaniwa Rais wa Ghana ameiona kabla ya kutoa amri ya kukamatwa kwa Nyantenkyi.
Kwesi Nyantenkyi amekuwa rais wa shirikisho la kandanda nchini Ghana tangu mwaka 2005 na hajatamka lolote.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.