Jumatatu November 28, Kocha mpya wa Yanga George Lwandamina ameanza majukumu yake kwa kuwaongoza wachezaji katika mazoezi kwa mara ya kwanza tangu atambulishwe kama kocha mkuu wa klabu hiyo.


Baada ya mapumziko ya muda mfupi, wachezaji wa Yanga wamerejea na kuanza mazoezi kwa ajili ya muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara inayotaji kuendelea katikati ya mwezi ujao.
Mazoezi hayo yamefanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kilwa Road Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo Hans van Pluijm alikuwepo pia katika mazoezi hayo pamoja na viongozi wengine wote wa benchi la ufundi waliokuwepo tangu wakati wa kocha huyo wa zamani.
Lwandamina atakuwa na kibarua cha kuiongoza Yanga kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara ambapo kwa sasa Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 15 za mzunguko wa kwanza.
Pia atapambana katika kuhakikisha Yanga inatetea taji la FA (Azam Sports Federation Cup) lakini pia katika michuano ya kimataifa (Caf Champions League).
No comments:
Post a Comment