Kuelekea mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya ligi mabingwa wa ulaya kati ya Porto dhidi ya Chelsea, katika dimba la Estadio de Dragao, mahasimu wawili watakutana kwa mara nyingine tena.
Kwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho na golikipa wa Porto Iker Casillas itakuwa zaidi ya mechi. Wawili hawa walikuwa mtu na kocha wake katika klabu ya Real Madrid, lakini uhusiano wao uliharibika kabisa wakati wote wakiwa Santiago Bernabeu.


Lakini Casillas, akiwa nahodha wa klabu yake na pia timu ya taifa, aliangalia kwenye picha kubwa na kuona hatari ya uhasama wa kwenye vilabu unaweza kuiathiri mpaka timu ya taifa.

Jambo hili lilionekana kama ni usaliti katika macho ya Jose Mourinho. Casillas alienda kuongea na maadui, mwisho wa siku akapoteza imani yake kwa Mourinho, na ukawa mwisho wa utawala wa himaya ya ‘mtakatifu Iker’ ndani ya Santiago Bernabeu.
Uhasama huo baina ya wawili hao ulichangia kukuza matatizo yaliyomuondoa Mourinho Madrid, na hata baada ya muda bado wawili hawa wameendelea kutupiana maneno – hivi karibuni wakati Casillas amejiunga na Porto – timu iliyowahi kufundishwa na Mourinho pia, mreno huyo hakuweza kukaa kimya, akaibuka na kusema mishahara ya Porto imemvutia Casillas kwenda Ureno.
No comments:
Post a Comment