Breaking News
recent

HUU NDIO MSIMAMO WA AZAM FC JUU YA TUKIO LA NYOSSO

Azam FC logoUongozi wa Azam FC umeketaa kuzungumza chochote kuhusu msimamo wao juu ya kitendo cha udhalilishaji alichofanya Juma Nyosso kwa mchezaji wao John Bocco kwakuwa jambo hilo tayari limeshafikishwa mikononi mwa TFF.
Msemaji wa Azam FC Jafar Idd Maganga amesema kuwa, waowamesikitishwa na kitendo hicho lakini baada ya TFF kutoa uamuzi wao, watatoa msimamo wao juu ya tukio lenyewe.
“Kitendo ambacho Juma Nyosso amekifanya kwa mchezaji wetu si cha kufurahisha katika mchezo wa mpira lakini vilevile ni kitendo cha udhalilishaji katika masuala ya kibinadamu”, amesema Jafar.
“Sisi kama Azam Football Club kwa sasa hatuna la kusema kwasababu TFF wamekuwa mbele kwenye suala hili, kwa ueledi waliokuwanao TFF hii ya Malinzi tunayoifahamu tunawaachia watoe maamuzi kutokana na tatizo hilo lakini pia tunamatumaini kuwa hawatachukua muda mrefu kuweza kutoa maamuzi dhidi ya kitendo hicho”.
“Sisi hatuwezi kuwaingilia, suala hili tayari lipo mikononi mwao ni sawa na kesi ambayo ipo mahakamani huwezi ukazungumza nje ya mahakama kwahiyo tunaiachia mahakama ikitoa maamuzi ndipo na sisi tutazungumza juu ya msimamo wetu”.
Juma Nyosso alimshika Bocco sehemu zake za makalio wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kati ya Azam FC dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi ambapo Azam FC ilishinda mchezo huo kwa goli 2-1.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.