Breaking News
recent

FAIDA ANAZOPATA CRISTIANO RONALDO NA UFALME WA SOCIAL MEDIA

cr7
Labda kazi ambayo Ronaldo hatumii nguvu sana bali akili yake na team yake ya management ni kwenye platform zake za mitandao ya kijamii. Hivi karibu nilikuandikia story ya kuonyesha watu maarufu kwenye soka wana-followers kiasi gani kwenye instagram. Neymar alikua namba moja lakini kwa ujumla mitandao yote ya kijamii hasa Facebook, CR7 anakua juu ya wenzake wote.
Ukurasa wa Ronaldo una likes 105,848,673 ambapo asilimia kubwa wapo active na wana-comment sana kwenye post zake. Mashabiki hawa wanatoka dunia nzima na Ronaldo ana wapa content kila siku.
Sasa hizi hapa ni njia ambazo CR7 anafaidika nazo kwa kuwa na ufalme kwenye mitandao ya kijamii.
1)Public Relation
Social Network ni njia pekee ambayo mashabiki wanaamini ujumbe huu umetoka kwa Cristiano Ronaldo na sio ulio-editiwa na waandhishi wa habari wala wakala wake. Hivyo basi mashabiki huwa wanaamini kwa asilimia kubwa maneno ya kwenye social media kutoka kwa Ronaldo zaidi hata ya ma-repoter.
The Sun walitoa interview ya maneno kuhusu CR7 lakini Ronaldo alitumia twitter kusema kwamba interview hiyo ni fake, hakufanya nao interview kwa hiyo wasisome. Mara moja mashabiki wa Ronaldo walipata ujumbe na kuipuuzia interview ile.
2)Financial Gain
Mwaka jana wataalam wa mahesabu na biashara ya mtandao walipiga mahesabu kwamba thamani ya post moja ya Cristiano Ronaldo ni $143,750 kwa brand ndogo na sio kubwa ambazo zina operate dunia nzima. Hivi sasa thamani hiyo imepanda mara dufu na inasemekana makadirio hayo yapo chini kwenye bei anayochaji Ronaldo ki uhalisia.Ronaldo amevuna pesa nyingi kutoka kampuni ya simu ya Samsung,Nike na nyinginezo kupitia page zake za social media tu.
3)To Activate Audience
Unaambiwa karibia 90% ya watu wanaom-follow Ronaldo akisema nunua Nike wananunua kweli, akisema nimeyapenda mashati yangu mapya ya CR7 basi wanaenda kununua kweli. Hadi kwenye majanga ya kidunia akihamasisha watu kutoa michango kusaidia wahanga mbalimbali, pale anaposema basi watu wengi hufanya hivyo.
4)Better Transfer and Contract Chances
Kwasababu club nyingi zipo kibiashara bila kusahau uwezo wa kucheza uwanjani. Mchezaji mwenye uwezo uwanjani na ushawishi mtandaoni kama Ronaldo inamsaidia sana kupata mkataba mzuri au uhamisho mkubwa sana.
5)Benefit After Pro Carrer
Umaarufu anaotengeneza kwenye social media unakua kila siku, hii inakua ni investment ambayo ataenda nayo hata akimaliza kucheza mpira. Bado kuna migahawa kama Subway inampa mkataba Pele kutokana na ushawishi wake wakiamini watafikia watu wengi. Hivyo basi familia ya Ronaldo kwenye social media inavyokua, hata akistaff na mshahara wa soka hauingii, ataendelea kupata pesa nyingi kupitia social media.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.