Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
‘Hii ni mara ya tatu Tanzania kupangwa kuanza na Uganda katika hatua ya mchujo ya CHAN katika misimu mitano iliyopita ya michuano hiyo.’
‘Hii ni mara ya tatu Tanzania kupangwa kuanza na Uganda katika hatua ya mchujo ya CHAN katika misimu mitano iliyopita ya michuano hiyo.’
Tanzania kwa mara ya tatu katika misimu mitano ya fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) itamenyana dhidi ya Uganda katika michuano hiyo mwakani (2016) nchini Rwanda.
Tanzania itaanzia nyumbani wikendi ya Juni 19-21 na kurudiana na Cranes wikendi ya Julai 3-5 nchini Uganda.
Tanzania (Taifa Stars) ilishinda kwa jumla ya mabao 3-2 dhidi ya Uganda katika msimu wa kwanza 2009, ikishinda 2-1 nyumbani na kutoka sare ya 1-1 jijini Kampala. Uganda ilikuwa shujaa mbele ya Tanzania mwaka jana 2014 katika kufuzu baada ya kushibda 1-0 ugenini na kushinda tena 3-1 kufuzu fainali zilizopita zilizofanyika nchini Afrika Kusini.
Kocha wa Cranes, Milutin ‘Micho’ Sredojević amesema Tanzania ni ngumu, lakini ameahidi kufanya kweli na kufuzu.
“Tanzania watakuwa wagumu, wachezaji wao wengi bado wanacheza ndani ya Tanzania, lakini hapa pia bado tuna wachezaji wazuri ambao walikuwapo katika CHAN iliyopita,” Micho amekaririwa na mtandao wa Kawowo Sports wa Uganda leo.
Wakati huo nchini nyingine za Ukanda wa CECAFA zimepangwa Djibouti kumenyana dhidi ya Burundi, Ethiopia dhidi ya Kenya
wakati Sudan inasonga mbele hadi hatua inayofuata kutokana na ubora wake wa soka.
wakati Sudan inasonga mbele hadi hatua inayofuata kutokana na ubora wake wa soka.
No comments:
Post a Comment