Na Anwar binde.
Kijana mmoja nchini Saudi Arabia alipiga picha binti huyu anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 10 akitafuta chakula katika pipa la taka taka kisha akaituma mitandaoni , kijana huyo aliweka maneno haya yenye kuudhi yakiashiria kuwadhihaki mashabiki wa Club ya Al Ittihad ya jeddah.
Baada ya binti huyo kuwa katika vazi la club hiyo ” Hapa ndio mashabiki wa Al Ittihad wanapostahili kuwepo” . Baada ya kuituma mitandaoni kijana huyo alipata shinikizo kubwa kutoka kwa jamii , siku chache baadae kijana huyo aliamua kurudi kwa binti huyo kumuomba msamaha akiwa na zawadi kadhaa .
Tukio hilo limepelekea shabiki mmoja tajiri wa Club ya al Ittihad kujitolea dola 16,000 kumsaidia binti huyo sambamba na mwanamichezo maarufu nchini Saudi Arabia dereva wa magari ya mashindano Yazeedi Al Rajhi kujitolea zaidi ya dola 100,000 kusaidia familia ya bint huyo. Kijana huyo alirudi katika mitandao ya jamii kuomba msamaha akiambatanisha na picha aliyopiga mara ya 2 na bint huyo .
Hii ndio selfie aliyojipiga kijana huyo na binti akitafuta chakula kwenye jalala
Na hii ndio picha aliyopiga baada ya kuomba msamaha na kumpelekea zawadi.



No comments:
Post a Comment