BINGWA wa dunia wa uzito wa kati asiyepigika, Danny Garcia anatarajia kupanda ulingoni kesho jumamosi Las Vegas Marekani kuchuana na Lamont Peterson katika pambano lisilo na ubingwa.
Mwaka 2012, Garcia alimpiga bila huruma Amir Khan katika raundi ya nne.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida jana wakati anahojiwa na kituo cha burudani cha TV cha MTZ, Garcia aliombwa kuonesha kitu cha pekee alichonacho mwilini mwake.
Bila kuwa na wasiwasi, bingwa huyo alieleza kuwa ana kidole cha ziada katika mguu wake wa kulia, akavua kiatu na kutoa soksi na kuonesha vidole sita alivyokuwa navyo.
Bondio huyo alisema kuwa na vidole sita ndio sababu ya kutopigwa hata siku.

10Apr2015
No comments:
Post a Comment