Breaking News
recent

Vurugu zasababisha mechi kuahirishwa

270FAF0300000578-3015247-image-a-35_1427497361736Na Augustino Mabalwe, Dar es salaam
Mechi kati ya Montenegro na Russia ya kutafuta tiketi ya kucheza Euro 2016 iliahirishwa hapo jana mara baada ya matukio kadhaa kutokea uwanjani
Awali sekundi ya 8 baada ya mpira kuanza kipa wa Russia Igor Akinfeev alipigwa na moto kichwani na kuzidiwa na hivyo nafasi yake ikachukuliwa na kipa Yuri Lodygin.
Tukio hilo lilifanywa na mashabiki wa Montenegro na kusababisa mwamuzi kusimamisha mchezo huo kwa muda mrefu na baaaye dakika ya 35 ukaendelea .
Hata hivyo kipindi cha pili mpira ulisimama kwa dakika 18 kufuatia vurugu za wachezaji wa pande zote 2 na makocha kutokana na mchezaji mwingine wa Russia kupigwa tena na moto.
Lakini baadaye dakika ya 66 mwamuzi aliamua kuahirisha mchezo huo baada ya kipa wa Montenegro Vukasin Poleksic  kuokoa penati ya Roman Shirokov
Mpaka pambano hilo lililopigwa nchini Montenegro linaahirishwa timu hizo zilikuwa hazijafungana.270FD62100000578-3015247-image-a-33_1427497321939
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.