Breaking News
recent

UWANJA GHALI ZAIDI KOMBE LA DUNIA WAGEUZWA KITUO CHA MABASI BRAZIL

                                      NA Sport nyumbani


 
Dunia ina mambo! Ule uwanja wa Mane Garrincha sasa unatumika kama sehemu ya madereva kubadilisha mabasi.



Mabasi ya abiria ya serikali zaidi ya 300 yamekuwa yakikutana kila siku kwenye uwanja huo kwa ajili ya madereva kubadilisha shifti.


Gazeti la The Mirror la Uingereza limesema uwanja huo wa pili kwa kuwa ghali zaidi katika historia ya soka duniani, sasa unatumika kwa kazi hiyo ambayo si yake.
WAKATI WA KOMBE LE DUNIA.
Serikali ya Brazil ilimwaga pauni milioni 350 kuutengeneza uwanja huo kwa ajili ya Kombe la Dunia mwaka jana na una uwezo wa kuingiza mashabiki 72,000 wakiwa wameketi.

Ndiyo uwanja ghali zaidi ukiwa wa pili baada ya Wembley wa Uingereza.

Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.