Breaking News
recent

Sepp Blatter akataa mdahalo wa moja kwa moja na Wapinzani wake

Sepp BlatterNa SPORT NYUMBANI
Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp
Blatter amekataa ombi la pamoja kutoka
mashirika ya habari ya BBC na SKY kushiriki
katika mjadala utakaokwenda hewani moja kwa
moja.
Wapinzani wake watatu wamekubali kushiriki
katika mjadala huo lakini wakasisitiza kuwa
wagombea wote ni sharti washiriki katika
mjadala huo kama mojawapo ya masharti.
Mapendekezo hayo ya BBC na SKY yaliwalenga
mashabiki ambao wamesema kuwa wanataka
kuwauliza maswali wagombea hao.
Uchaguzi wa rais wa shirikisho la FIFA
unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 29 mwezi
Mei mjini Zurich.
Wagombea wengine katika uchaguzi huo wa FIFA
ni rais wa shirikisho la soka nchini Jordan Ali Bin
Al Hussein,Rais wa shirikishp la soka nchini
Uholanzi Michaek Van Praag na aliyekuwa
mchezaji wa Barcelona Louis Figo.
Blatter mwenye umri wa miaka 79 anataka
kuliongoza shirikisho hilo kwa muhula wa tano.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.