Breaking News
recent

Ronaldo aongoza kuwa kusanya wafuasi Facebook

Real Madrid forward Cristiano Ronaldo gestures to fans before their soccer friendly match against the Los Angeles Galaxy in PasadenaMchezaji nyota wa Real Madrid ya Uhispania na Ureno Christiano Ronaldo ndiye binadamu maarufu zaidi duniani kwenye Facebook.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30
amempiku Mwanamuziki maarufu kwa kunengua
kiuno Shakira nawafuasi zaidi ya milioni 107.
Ronaldo anawafuasi 107,096,356 wakilinganishwa na 107,087,100 Shakira Ronaldo aliweka rekodi kwa kuwa mchezaji maarufu zaidi duniani alipotimiza wafuasi milioni 100 mwezi Oktoba mwaka uliopita.
Nyota huyo wa Real Madrid alijiunga na mtandao
wa kijamii wa Facebook mwaka wa 2009.
Na si hapo alikodhibitisha udedea wake, Ronaldo
anazaidi ya wafuasi milioni 34 katika mtandao
wa kijamii wa Twitter ambako anaorodheshwa
katika nafasi ya 13.cristiano_ronaldo_facebook
Ronaldo anawafuasi 107,096,356 Msanii h Katy Perry ndiye anayeongoza kwa umaarufu kwenye twitter akiwa na jumla ya wafuasi milioni 66.6.
Justin Bieber, Barack Obama, Taylor Swift, YouTube, Lady Gaga, Justin Timberlake, Rihanna, Britney Spears, Ellen DeGeneres, Instagram na Twitter ndio wanaompiku  Ronaldo.
Licha ya hiyo yeye ndiye mwanaspoti maarufu
zaidi kwenye mtandao huo wa Twitter.
Mshambulizi wa Brazil na Orlando City Kaka
ndiye mchezaji wa pili kwa umaarufu akiwa na
wafuasi milioni 22.2 million.
Ronaldo ndiye mchezaji maarufu zaidi duniani
Licha ya kuwa maarufu na wafuasi wa timu ya
Uingereza ya Manchester United kiungo
machachari Wayne Rooney anashikilia nafasi ya
95 katika mtandao huo akiwa na wafuasi milioni
10.8 million.
Katika Facebook hata hivyo, Mchezaji bora mara
nne duniani na Mshambulizi wa Barcelona ,Lionel
Messi ndiye mwanaspoti wa pili kwa umaarufu
duniani.
Messi anawafuasi milioni 78.
Nyota wa zamani wa England David Beckham
anafunga orodha ya tatu bora kwa wafuasi
milioni 52 .
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.