Breaking News
recent

PACQUIAO SASA AJIFUA NA MBWA WAKE KATIKA MITAA YA LOS ANGELES, MAREKANI

Manny Pacquiao anaonyesha kweli hataki mchezo kabla ya pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather Jnr litakalopigwa Mei 2, mwaka juu.


Bondia huyo maarufu kama Pacman,  amekuwa akifanya mazoezi katika mitaa ya jiji la Los Angeles nchini Marekani kwa siku ya tatu mfululizo.

Jana aliongozana na mbwa wake pamoja na timu yake ya ufundi, mazoezi yalianza saa 11:30 alfajiri.
Baada ya hapo alitoa shoo kwa kupiga ngumi huku na kule kuonyesha kwamba anataka kutoa somo kwa Mayweather ambaye hajawahi kupigwa.

Hilo pambano ndiyo ghali zaidi la ngumu na Mayweather ataibuka na pauni milioni 150 huku Pacquiao akipata pauni milioni 100.






Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.