MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah amewatumia ujumbe klabu yake, Chelsea baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 wa klabu yake ya mkopo, Fiorentina dhidi ya Juventus usiku wa jana.
Kwa mabao hayo katika Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Italia, Salah sasa anafikisha jumla ya mabao sita katika mechi saba.
Mabao hayo ya Salah aliyofunga dakika za 11 na 60, yanaifanya Juventus ipoteze mechi ya kwanza nyumbani baada ya mechi 48.
Lazio imetoka sare na Napoli ya kufungana bao 1-1 katika Nusun nyingine ya Kombe la Mfalme na mechi za marudiano zitafanyika Aprili 7 na 8.

Mohamed Salah akimtoka mchezaji wa Juventus kabla ya kufunga bao la kwanza

Mwanasoka huyo wa kimataifa akishangilia oja ya mabao yake jana
REKODI YA MABAO YA SALAH
BASLE: Mechi 67, mabao 3.
CHELSEA: Mechi 19, mabao mawili.
FIORENTINA: Mechi saba, mabao sita
EGYPT: Mechi 35, mabao 20.
No comments:
Post a Comment