Breaking News
recent

Matumla kucheza kwa Pacquiao

BONDIA, Mohamed Matumla, ametajwa kucheza pambano la utangulizi kusindikiza pambano la nguli wa masumbwi duniani, Manny Pacquiao na Floyd Mayweather litakalofanyika Mei 2 jijini Las Vegas, Marekani.
Matumla Jr ametajwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Dunia (WBF) kucheza pambano hilo kwa sharti la kushinda pambano lake la Machi 27 dhidi ya Wang Xin Hua wa China litakalofanyika Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Pambano la Matumla Jr na Hua limepangwa kuwa la raundi 12 la uzani wa bantam na bingwa atatwaa mkanda wa dunia wa (WBO Eliminate Tittle).
Bingwa wa zamani wa dunia wa uzani wa juu, Francois Botha, ametajwa kuwa mgeni rasmi kwenye pambano hilo ambapo pia bondia wa uzani wa juu hapa nchini, Ashraf Suleiman atazichapa na Joseph Rabotte wa Marekani.
Promota wa pambano hilo, Jay Msangi alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na pambano litasimamiwa na WBF ambaye rais wake atawasili nchini Machi 21.
Wakati huohuo, bingwa wazamani wa dunia wa WBU, Rashid Matumla ambaye ni baba na kocha wa mwanaye, Matumla Jr, ametamba kuwa anaamini mwanaye hawezi kumwangusha.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.