
Meneja wa timu ya Manchester United Louis Van Gaal amesema kwamba winga Muargentina wa timu hiyo Angel Dimaria ataendelea kuwa sehemu ya kikosi hicho.
Kiwango dhaifu alichokionesha katika mchezo wetu na Arsenal tuliopoteza kwa goli 2-1 kwenye kombe la FA imesababisha kuleta uvumi mwingi kuwa mchezaji huyo atauzwa ili tusiwe naye tena hapa Old Trafford.
Louis Van Gaal alizidi kusema kuwa “Nadhani atabakia, mwenendo wake hadi sasa mara baada ya kufungwa na Arsenal pia kadi nyekundu aliyoipata unaonekana kuwa nzuri.
Angel Dimaria (27) alisaini mkataba na Manchester United mwaka jana mwezi wa 8 na hadi sasa hajafunga goli hata moja licha ya kusaidia magoli matatu katika mechi zake 10 za mwisho tokea December 1 mwaka jana
Licha ya hayo Van Gaal amekuwa akilalamikiwa sana juu ya mfumo wake mpya ambao amekuwa akiutumia tangu ajiunge na mashetani hao wekundu huku akisema akiwa na imani ya kufanikiwa ndani ya miaka mitatu kitu ambacho kimekuwa kigumu sana.
No comments:
Post a Comment