Dereva wa mbio za magari za langalanga Muingereza Lewis Hamilton ametawala mbio za Australian Grand Prix na kufanikiwa vyema kutetea taji lake la ubingwa wa dunia.
Hamilton aliendesha vyema na kumudu kuacha pengo dhidi ya dereva mwenzake wa timu ya Mercedes, Nico Rosberg katika muda wote wa mbio hizo huku wakiwaacha washiriki wengine nyuma.
Katika mbio hizo dereva mpya wa timu ya Ferrari, Sebastian Vettel alizinduka na kuongeza mwendo na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kumpita dereza wa timu ya Williams Felipe Massa.
Lewis Hamilton akimwaga Champagne kushangilia ushindi wake.
Lewis Hamilton alijikuta akipatwa na mshangao baada ya Arnold Schwarzenegger kujitokeza na kuanza kufanya mahojiano naye.
No comments:
Post a Comment