
Kelvin Yondani amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 watakaoivaa BDF XI, ya Botswana Jumamosi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika
BEKI wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 watakaoivaa BDF XI, ya Botswana Jumamosi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupona maumivu ya kifundo cha mguu yaliyomweka nje kwa wiki mbili.Daktari wa Yanga Juma Suphian ameiambia Goal Yondani yupo katika hali nzuri na ameanza kufanya mazoezi na wenzake siku nne zilizo pita tangu kumaliza kwa mechi ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar Jumapili iliyopita na kilicho baki ni maamuzi ya kocha Hans Pluijm kama atamtumia.
“Yondani yupo fiti kwa sasa na anaweza kuwepo kwenye mchezo wetu wa Jumamosi wa kombe la Shirikisho dhidi ya BDF XI ya Botswana na nimchezaji mmoja tu ambaye atakosa mchezo huo Edward Charles ambaye ameumia kwenye mechi yetu na Mtibwa Sugar,”amesema Suphian.
No comments:
Post a Comment