Breaking News
recent

Shabiki: Sijamgomea Kenyatta




SHABIKI sugu wa Gor Mahia, Jaro Soja, ambaye hivi majuzi aliandamana na kikosi cha K’Ogalo hadi Ikulu kwa Rais Uhuru Kenyatta wakati timu hiyo ilipopongezwa kwa kutetea taji la Ligi Kuu Kenya, amepiga taarifa za kukataa kazi aliyopewa na kiongozi huyo wa nchi.
Jared Otieno mwenye umri wa miaka 34, ameelezea kushitushwa na habari hizo kwamba ameigomea kazi aliyopendekezwa na Rais ya kujumuishwa kwenye bodi inayosimamia viwanja vya humu nchini, SSMB.
“Nimeshitushtwa kusikia taarifa kuwa nimekataa kazi niliyopewa na Rais Uhuru Kenyatta. Makubaliano kati yangu na Rais ilikuwa kwamba nikutane na Waziri wa Michezo (Dkt Hassan Wario) na vile vile Mwenyetiki wa mfuko wa vijana, Uwezo Fund (Nick Odhiambo) ili waone sehemu watakayonipanga,” alisema Soja.
Ni kwenye ziara hiyo ambapo wachezaji wa Gor walimkabidhi Rais Kenyatta jezi yenye jina lake ikiwa na nambari 01.
Kwa upande wake, kiongozi huyo wa taifa aliizawadia timu hiyo Sh1 milioni papo hapo na kuwaahidi kuwaongezea kibunda kingine cha Sh2 milioni kwa ajili ya kuwapiga jeki kwenye matayarisho yao ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika za mwakani. Pia aliahidi kuitafutia wadhamini.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.