
UONGOZI wa klabu ya Yanga umekubaliana kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja kocha wake raia wa Uholanzi Hans van der Pluijm
UONGOZI wa klabu ya Yanga umekubaliana kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja kocha wake raia wa Uholanzi Hans van der Pluijm, baada ya kuridhishwa na kiwango chake cha ufundishaji na kiwango kinachoonyeshwa na timu yao katika michuano yote inayoshiriki.Msemaji wa Yanga, Jerry Muro, ameiambia Goal, Pluijm amekibadilisha kwa asilimia kubwa kikosi chao na kucheza soka la kuvutia tofauti na wakati ule ilipokuwa inanolewa na Mbrazili Marcio Maximo aliyetimuliwa baada ya kufungwa na Simba kwenye mchezo wa Nani Mtani Jembe.
“Tumeona tumuongezee mkataba kocha wetu kwa sababu tumeona mafanikio katika kipindi ambacho timu imekuwa chini yake kwa sasa tunaongoza ligi ya Tanzania lakini pia tumeshinda mchezo wetu wa kwanza wa michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF ya Botswana Jumamosi iliyopita,”amesema Jerry Muro.
Pluijm aliyekuwa akiifundisha klabu ya Berekum Chelsea ya Ghana, amekuwa na rekodi nzuri tangu alipoanza kuifundisha Yanga msimu uliopita na mara aliporejea msimu huu bado mambo yameweza kumwendea vyema kutokana na kuwa na mwenendo mzuri tangu alipoichukua timu hiyo Desemba 2015.