Mrisho Ngassa yupo katika hatua za mwisho kuongeza mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo aliyoipenda toka utotoni
WINGA machachari wa Yanga Mrisho Ngassa yupo katika hatua za mwisho kuongeza mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo aliyoipenda toka utotoni kwake baada ya uongozi wa timu hiyo kuamua kumlipia deni lililokuwa lina msumbua na kusababisha kushuka kiwango chake.
Baada ya kumalizana na uongozi wa Yanga Ngasa ameiambia Goal kwa sasa hana tena kinyongo na yupo tayari kuipigania timu yake ili kuipa mafanikio kama alivyo fanya msimu uliopita kwa kuwa mfungaji bora kwenye ligi ya Mabingwa Afrika.
"Naomba mashabiki wa Yanga waje kwa wingi uwanjani Jumamosi tutakapo kuwa tunacheza na BDF XI ya Botswana kujionea kiwango kitu nitakacho wafanya kwa sasa nipo fiti sina tena kinyongo baada ya kualizana na viongozi wangu,”amesema Ngassa.