Breaking News
recent

MAPEMAAAA....PACQUIAO AANZA KUJIFUA ILI KUMVAA MAYWEATHER

 Manny Pacquiao mapemaaa, ameanza mazoezi kujiandaa na pambano la Mei 2 dhidi ya Floyd Mayweather ambaye hajawahi kupigwa.


Pambano hilo linaloaminika kuwa ghali zaidi duniani katika mchezo wa ngumi, litapigwa jijini Los Angeles, Marekani.

Tayari Manny ameanza kujifua katika kisiwa cha Mindanao Kusini kwao Ufilipino.

Uamuzi wa kuanza mapema umeifanya dunia iamini, Mfilipino huyo ambaye sasa ni mwanasiasa kwamba amepania kuionyesha dunia.




Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.