Breaking News
recent

Kibuti Kumbe Ronaldo ndiye alitoswa na Irina

ACHANA na mapenzi. Unaweza kuwa na pesa, umaarufu na uzuri wa sura lakini vitu hivyo visiwe kila kitu katika penzi lako.
Cristiano Ronaldo akajipange upya. Ni kweli kuwa ana vitu hivyo vitatu huku pia akiwa ni mwanasoka bora wa dunia, lakini hayo hayamhusu Irina Shayk.
Hivi majuzi imebainika kwamba mrembo huyo wa Kirusi ndiye aliyemtosa Ronaldo katika penzi lao lililodumu kwa miaka mitano tofauti na mitazamo ya watu kwamba huenda Ronaldo ndiye aliyemtosa Irina.
Baada ya kukaa kimya, Irina ametoboa siri hiyo kwa kujibu kwa mafumbo wakati alipoulizwa ni aina gani ya mwanaume mpya anayemtaka; “Napenda wanaume waaminifu na nampenda mwanamume ambaye anabakia kuwa mkweli kwa wanawake.”
Kwa mujibu wa jarida maarufu la HELLO ambalo linaloshughulika na maisha ya mastaa wa fani mbalimbali, imebainika kuwa alikuwa ni Irina ambaye aliamua kuhitimisha uhusiano wake na Ronaldo katika jumba lao la kifahari jijini Madrid wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya.
“Irina alikuwa katika mshangao na alifadhaika sana. Haukuwa uamuzi aliouchukua kirahisi,” alisema rafiki mmoja wa karibu wa Irina.
“Aliondoka haraka na kwenda katika Sikukuu ya Mwaka Mpya akilia peke yake katika uwanja wa ndege kabla ya kupaa kwenda Maldives na alisherehekea siku yake ya kuzaliwa peke yake,” aliongeza rafiki huyo.
Ulikuwa ni mwisho wa haraka kwa mastaa wawili waliokuwa na nguvu sana. Irina pia alikuwa amejipa jukumu la kuwa mama wa kambo wa mtoto wa kiume wa Ronaldo, Cristiano Jnr, ambaye alizaliwa muda mfupi baada ya wawili hao kuanza uhusiano mwaka 2000.
“Irina siku zote aliamua kumtetea mwanaume wake,” anaongeza shosti huyo ambaye hata hivyo alidokeza kwamba maji yalimfika shingoni mrembo huyo wa Kirusi.
“Kulikuwa hakuna jinsi na ukweli ulikuwa unamtazama katika macho yake.
Baada ya kufikiria sana aliona kwamba kulikuwa hakuna jinsi ambavyo angeweza kupuuzia mambo,” aliendelea rafiki wa Irina kutoboa ukweli.


Kutokana na uamuzi huo mgumu, Irina aliamua kutoendelea kuwa mmoja kati ya wafuasi wa Ronaldo katika Mtandao wa Twitter huku pia akifuta picha zote za staa huyo wa Real Madrid katika mtandao wake wa Instagram. Badala yake aliamua kuweka picha zake mwenyewe akiwa anakula raha katika Kisiwa cha Maldives ‘kuonyesha dunia kwamba ameamua kuwa peke yake’.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.