Breaking News
recent

Coutinho ataka kasi zaidi ya mabao




KIUNGO wa Yanga, Andrey Coutinho, amesema kuwa ushindi wanaopata kwenye Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho ni mdogo na badala yake amesema wanatakiwa kucheza mpira wa kasi ili kupata mabao mengi zaidi.
Coutinho alisema: “Kocha anafanya kazi kubwa, sisi wachezaji pia tunafanya hivyo hivyo. Nafikiri tukicheza mpira wa kasi zaidi kuliko ilivyo sasa tutaweza kufanya vizuri na hata kupata mabao mengi.
“Kuna wachezaji kama Msuva (Simon), Ngassa (Mrisho), Sherman (Kpah) na Niyonzima (Haruna) ambao wanaweza kupanda na kushambulia kwa kasi kubwa na huku wengine kwenye timu wakifanya kazi ya kumalizia.
“Naamini tukijaribu hilo, tutaweza kufanikiwa kwa kuwa wachezaji wengi tunaocheza dhidi yao hawana kasi kubwa na badala yake tutaweza kuwazidi kwa kupata matokeo mazuri.”
Coutinho amekuwa akitamba kwenye kikosi cha kwanza cha Kocha Hans Van Pluijm kama ilivyokuwa enzi za Mbrazili, Marcio Maximo.
Sport Nyumbani

Sport Nyumbani

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.