Klabu ya Barcelona imeonyesha heshima kubwa kwa kuupa uwanja wake wa mazoezi wa timu kubwa jina la 'Camp Tito Vilanova'.
Klabu hiyo imeamua kufanya hivyo ikiwa ni heshima kwa aliyekuwa kocha wake, Tito Vilanova aliyefariki dunia mwaka jana kutokana na ugonjwa wa kansa.
![]() |
VILANOVA (KULIA) WAKATI WA UHAI WAKE ALIPOKUWA KOCHA MSAIDIZI CHINI YA PEP GUARDIOLA. |
Wachezaji wote, viongozi pamoja na familia ya Vilanova walikuwa uwanjani hapo wakati wa shughuli hizo za kutangaza jina hilo rasmi.
No comments:
Post a Comment