Azam imebadilisha muda wa kufanya mazoezi na sasa kinafanya mazoezi kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 8 mchana ili kuzoea hali ya joto ambalo watakumbana nalo Khartoom
KIKOSI cha timu ya Azam kimebadilisha muda wa kufanya mazoezi na sasa kinafanya mazoezi kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 8 mchana ili kuzoea hali ya joto ambalo watakumbana nalo Khartoom watakapo kwenda kurudiana na Al Merreikh ya Sudan kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAF.
Kocha wa Azam FC Joseph Omog ameiambia Goal, lengo la kufanya hivyo ni kutaka wachezaji wake kuizoea hali hiyo ya Joto na kuweza kupambana kwa dakika zote 90 kulinda ushindi wao walioupata Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Azam Complex.
“Bado tunakazi kubwa kuhakikisha tunasonga mbele wapinzani wetu Al Merreikh,ni timu nzuri na watafanya kila mbinu ili kutufunga nandio sababu nataka tujiandae kwa kila namna ili tuweze kufanikiwa,”amesema Omog.
Azam inatarajia kuelekea Sudani siku mbili kabla ya mchezo huo uliopangwa kuchezwa Khartoom February 28 kwenye uwanja wa Al Merreikh huko Sudan Kaskazini.