Wenyeji Azam wamekuwa na maandalizi kabambe kujiandaa na michuano hiyo hivi karibuni ilikwenda kupiga kambi ya wiki moja DR Congo
AZAM FC kesho Jumapili itakuwa na kibarua kigumu itakapo wakaribisha Al-Merrikh, ya Sudan katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakao fanyika kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Timu hizo zinakutana kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza Azam ilifungwa kwa mabao 4-3 kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa robo fainali wa michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika Kigali Rwanda Julai 2014.
Wenyeji Azam wamekuwa na maandalizi kabambe kujiandaa na michuano hiyo hivi karibuni ilikwenda kupiga kambi ya wiki moja DR Congo na kucheza mechi tatu za kirafiki na timu za TP Mazembe, Zesco United na Don Bosco.
Lakini pia timu hiyo inayoongoza ligi ya Tanzania bara kwa sasa ipo kwenye kiwango bora kutokana na uimara wa kikosi ilichokuwa nacho ambacho kinaundwa na wachezaji kutoka mataifa ya Ivory Coast, Uganda ,Burundi na Tanzania.
Kocha wa Azam Mcameroon Joseph Omog, ameimabia Goal anaifahmu vizuri Al-Merrikh, ni timu nzuri na tajiri Afrika lakini wamejipanga kuhakikisha wanapambana nayo na kupata ushindi katika mchezo huo aliouita mgumu.
“Tumejipanga kuhakikisha tunashinda najua Al-Merrikh,ni timu imara inawachezaji wenye viwango vya juu lakini hatuwaogopi tumejiandaa kuhakikisha tunacheza vizuri na kushinda mchezo huo wa keshi ili kutimiza malengo yetu,”amesema Omog.
Omog amesema atatumia kikosi kile kilichocheza mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo walishinda mabao 5-2, huku tegemezi lake kubwa katika mabao likiwa ni Didier Kavumbagu na Kipre Tchetche ambao kwa sasa ndio vinara katika ufungaji kwa timu hiyo inayoongoza ligi ya Tanzania bara ikiwa na pointi 25.
Kwaupande wao Al-Merrikh, tayari wamewasili Tanzania wakiwa na matumaini makubwa ya kuondoka Tanzania na ushindi kutokana na ubora wa kikosi chao na kocha wao Otto Pfister amesema wenyeji wao nitimu dhaifu ambayo haiwezi kuwanyima usingizi.
Kocha huyo ameiambia Goal kuwa Azam ni timu change katika soka la Afrika na hatarajii kupata changamoto zaidi ya ushindi ambao anauhakika watashinda .
“Nimekuja na kikosi changu kamili kwa sababu nataka kumaliza kazi huku huku na kujipanga na mchezo wa raundi inayofuata,”amesema Pfister.
Mmoja wa wachezaji anayewapa hofu Azam ni mshambuliaji raia wa Mali Mohamed Traore aliyekuwa akitakiwa na Azam kwenye dirisha dogo la usajili lakini mshambuliaji huyo aligoma kutua kwa matajiri hao kutokana na dau kubwa alilopewa na klabu hiyo.